Milipuko miwili imetokea katika uwanja wa ndege wa Zaventem mjini Brussels.

BRUSSELS UBELGIJI

Milipuko miwili imetokea katika uwanja wa ndege wa Zaventem mjini Brussels.Moshi ulionekana ukitanda angani kutoka kwa moja ya majengo katika uwanja huo.Watu 13 wameripotiwa kuua na wengine 35 kujeruhiwa.Watu wameondolewa kutoka kwenye uwanja huo na safari za ndege kutua au kupaa kutoka uwanja huo kukatizwa.

Mshukiwa wa Paris alitaka kujilipuaVyombo vya habari nchini humo vinaripoti kwamba kuna watu wamejeruhiwa katika ukumbi wa kuhudumia watu wa safari za kuondoka nchini na kwamba milipuko ilitokea karibu na meza ya shirika la ndege la American Airlines.

Haijabainika ni nini chanzo cha milipuko hiyo.Milipuko pia imeripotiwa katika kituo cha treni cha Maelbeek karibu na majengo taasisi za Umoja wa Ulaya. Mfumo wa uchukuzi wa treni mjini Brussels umefungwa.

Milipuko hiyo imetokea siku nne tu baada ya kukamatwa kwa mshukiwa mkuu wa mashambulio ya Paris ya mwaka jana ambayo yalisababisha vifo vya watu 130.Abdeslam alikamatwa Ijumaa katika mtaa mmoja wa Brussels.

Uwanja wa ndege wa Zaventem unapatikana kilomita 11 kaskazini mashariki mwa Brussels na ulihudumia abiria zaidi ya 23 milioni mwaka jana.

Comments

comments

Random Posts