Miamba wa Uhispania Barcelona wamepokea kichapo cha tatu mfululizo katika ligi ya La Liga baada ya kulazwa na 2-1 Valencia nyumbani kwao Jumapili.

Miamba wa Uhispania Barcelona wamepokea kichapo cha tatu mfululizo katika ligi ya La Liga baada ya kulazwa na 2-1 Valencia nyumbani kwao Jumapili.

Hii ni mara yao ya kwanza kushindwa mechi tatu mfululizo ligini tangu 2003.

Kitulizo pekee kutoka kwa mechi  hiyo ni kwamba mshambuliaji wao matata Lionel Messi alifunga bao lake la 500.

Ivan Rakitic aliingiza wavuni krosi iliyotoka Guilherme Siqueira na kuwapatia Valencia uongozi wa kushangaza.

Santi Mina baadaye alifunga bao la pili dakika za mwisho za kipindi cha kwanza.

Barcelona sasa wanaongoza ligi kwa kuwa wamefunga mabao mengi kushinda Atletico Madrid.

Barca wana alama 76 na tofauti ya mabao 59 nao Atletico wana alama sawa lakini tofauti ya mabao 41.

Real Madrid wamo nambari tatu na alama 75 na mabao 68. on goal difference.

Barcelona, chini ya mkufunzi wao Luis Enrique, walianza mwezi Aprili wakiwa alama tisa mbele ya Atletico lakini uongozi huo umefutika upesi.

Walianza kwa kushindwa na Real Madrid kwenye El Clasico.

Aidha, Atletico waliwaondoa kwenye Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya wiki iliyopita.

Barca huenda wakaondolewa kileleni iwapo watashindwa kupata ushindi ugenini Deportivo La Coruna Jumatano.

Atletico watakuwa ugenini Athletic Bilbao siku hiyo nao Real Madrid nyumbani dhidi ya Villarreal.

Comments

comments

Random Posts