Mhalifu wa kivita afariki baada ya kunywa sumu mahakamani The Hague

Sumu

Kikao cha kusikiliza rufaa iliyowasilishwa na washtakiwa wa uhalifu wa kivita mjini The Hague, Uholanzi kimesitishwa ghafla baada ya mmoja wa washtakiwa kusema amekunywa sumu baada ya kusikiliza hukumu.

Slobodan Praljak, 72, alikuwa mmoja wa viongozi sita wa zamani wa kisiasa na wa kijeshi wa Bosnia wa asili ya Croatia ambao walikuwa wamefika mahakamani.

Amefariki akitibiwa hospitalini na Umoja wa Mataifa umesema sasa mahakama hiyo ni “eneo la uhalifu”.

Alikuwa amehukumiwa kufungwa jela miaka 20 mnamo 2013 kwa makosa ya uhalifu wa kivita yaliyotekelezwa katika mji wa Mostar.

Baada ya kusikiliza hukumu kwamba majaji walikuwa wamedumisha kifungo hicho, alimwambia jaji, “Nimekunywa sumu”.

  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments