Mfumuko wa Bei Umeongezeka Kwa asilimia 1.4 Ikilinganishwa na Ongezeko la Asiliia 1.0

BEI

Mfumuko wa Bei wa mwezi March 2017 Unaopimwa Kwa Kipimo Cha Mwezi Umeongezeka Kwa asilimia 1.4 Ikilinganishwa na Ongezeko la Asiliia 1.0 Kwa Mwezi February 2017. Kwa Mujibu wa Taarifa ya Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa Takwimu Farihisi za bei Zimeongezeka hadi 108.44 Mwezi March 2017Kutoka 106.97 Mwezi February 2017.

Taarifa imesema kuongezeka kwa farihisi za bei kumchangiwa na kuongezeka kwa bei bidhaa za vyakula na kutaja baadhi ya vyakula vilivyochangia kuongezeka kwa farihisi ni pamoja na mchele kwa asilimia 4.7, Sukari asilimia3.9 ,Unga wa mahindi asilimia 6.7 na mtamakwa asilimia 4.1

Pamoja nan a Hayo ndizi za Kupikiaa kwa asilimia 7.7, mihogo mibichi kwa asilimia 4.0 na dagaa kwa asilimia 3.2

Aidha taarifa hiyo imebainisha baadhi ya Bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa mfumuko wa bei ni pamoja na gesi ya kupikia majumbani kwa asilimia 11.9, Petoli kwa asilimia 4.6 na dizel kwa asilimia 3.2.

Mwandishi: Tuse Kasambala

#SIBUKAMEDIA

Comments

comments

Random Posts