Mchezaji wa Cameroon afariki akiwa uwanjani

ekeng8s-3-web
Mchezaji Patrick Ekeng wa Cameroon anayechezea timu ya Dinamo Bucharest , amefariki baada ya kuanguka uwanjani akicheza ligi ya Romania.Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alipoteza fahamu dakika saba tu baada ya kuingia uwanjani kuchukua nafasi ya mchezaji mwingine katika mji mkuu wa Romania, Bucharest.

Taarifa zinasema matabibu walimkimbiza hospitalini ambako madaktari walijaribu kumfufua kwa zaidi ya saa moja bila kufaulu.

Haijajulikana ni nini kilisababisha kifo chake na hakuwa amegusana wala kukaribiana na mchezaji mwingine alipoanguka uwanjani.

Comments

comments