Mbunge wa IRINGA MJINI kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA),Mchungaji PETER MSIGWA ameachiwa na polisi mkoani humo baada ya kukamatwa siku ya jumapili.

Mbunge

Mbunge wa IRINGA MJINI kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA),Mchungaji PETER MSIGWA ameachiwa na polisi mkoani humo baada ya kukamatwa siku ya jumapili.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa msemaji wa CHADEMA,TUMAINI MAKENE, mbunge huyo alikamatwa wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika eneo la MLANDEGE huko Mkoani IRINGA.

Kwa mujibu wa MAKENE,Mchungaji MSIGWA amekamatwa kwa kosa la kufanya uchochezi wakati akihutubia mkutano huo ambao ulihudhuriwa na wafuasi wa CHADEMA mkoani IRINGA.

Hata hivyo mbunge huyo ambae pia ni mchungani wa kanisa,atatakiwa kuripoti kituo cha polisi mkoani humo siku ya jumatatu.

  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments