MAULID MTULIA ametangaza kuhamia CCM.

Siku chache baada ya aliyekuwa mbunge wa KINONDONI kupitia Chama cha Wananchi CUF,MAULID MTULIA kutangaza kukihama chama hicho na kuhamia CCM,CUF kimesema ameonda uaminifu kwa wanachama wake.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini DAR ES SALAAM,

Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma CUF, ABDUL KAMBAYA amesema ameondoa uaminifu kwa wana KINONDONI kwa kuwa wananchi walimwamini na hata kulala nje wakipigania kuraa zake za ubunge huku wengine wakiumizwa na kufikishwa mahakamani lakini yeye amewasaliti.

Amesema kuwa MTULIA amekitia doa chama hicho kutokana na matando yake aliyoyafanya kwa wananchi na chama kwa ujumla huku akisema kuwa sababu za kuhama kwake hazina mashiko.

 #SIBUKAMEDIA

 

 

Comments

comments