Mauaji yatokea Tabora.

tabora
Watu wanne wamekufa katika matukio tofauti mkoani TABORA likiwemo la mtu mmoja kujinyonga kwenye  nyumba ya kulala wageni iliyopo kata ya CHEMCHEM mjini TABORA.
Kamanda wa polisi mkoani TABORA,Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa polisi WILBROAD MUTAFUNGWA amesema katika tukio la kwanza mtu mmoja mkazi wa kijiji cha KIYOMBO wilayani SIKONGE ameuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani.
Katika tukio la pili kamanda MUTAFUNGWA amesema mtu mmoja mkazi wa kijiji cha SHITAGE wilayani UYUI ameuawa kwa kukatwakatwa na mapanga shingoni na watu wasiofahamika.

Kamanda wa polisi mkoa wa TABORA pia amesema katika tukio la tatu, mtu mmoja mkazi wa mkoa wa MWANZA amekufa kwa kujinyonga katika nyumba ya kulala wageni ya MLELA iliyopo kata ya CHEMCHEM katika Manispaa ya TABORA.

Ameeleza kuwa katika kijiji cha UTULA,kata ya MABAMA wilayani UYUI mtu ameuawa kwa kupigwa kwa fimbo na kuchomwa na kitu chenye ncha kali kidevuni huku chanzo kikiwa ni kuwania mali.

Amewataka wananchi kushirikiana na jeshi la polisi kwa kutoa taarifa za watu wanaowahisi kuhusika na uhalifu ili kukomesha vitendo vya mauaji.

  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments