Mauaji ya kinyama yafanyika DR Congo

images

Takriban watu 22 wameuwawa kutokana na mashambulio yaliyofanywa na kundi la wapiganaji wenye itikadi kali za Kiislamu katika eneo la Mashariki ya Kongo.

Mashambulio hayo yamefanyika katika mji wa Eringeti uliopo kwenye jimbo la Kivu Kaskazini. Kwa mujibu wa mchungaji mmoja wa Kanisa katoliki baadhi ya watu waliuwawa kwa kuchomwa visu na wengine kwa kupigwa risasi.

Mchungaji huyo amelishutumu kundi hilo la ADF la wapiganaji wa Kiislamu wenye itikadi kali kuhusika na mashambulio hayo. Kundi hilo lilianzishwa nchini Uganda manamo mwaka 1995 na limewauwa mamia ya watu katika miaka ya hivi karibuni.

#DW SWAHILI

Comments

comments

Random Posts