Marufuku nguo za kubana Chuo Kikuu cha Lagos.

LAGOS

Chuo kikuu cha Lagos nchini Nigeria kimepiga marufuku wanafunzi kuvaa nguo zinazobana mwili.

Taarifa iliyotolewa kwa wanafunzi chuoni hapo inasema wanapaswa kuonekana nadhifu wawapo katika maeneo ya chuo, na kwamba uvaaji wa nguo za kubana ama zinazoonesha miili yao, sio jambo la kufaa.

Chuo kimepiga marufuku nguo zote ambazo zinaonesha maeneo nyeti ya sehemu za mwili kama vile kifua, tumbo, sehemu ya matiti, makalio.

Raia wengi wa Nigeria wamekuwa wakipendelea kuvaa nguo zenye staha, lakini katika kizazi cha vijana wa sasa mara mara nyingi wamekuwa wakidharau maadili ya mavazi ya asili.

#SIBUKAMEDIA

Comments

comments