Manispaa ya Dodoma, Imeshutumiwa na Madiwani wa Halmashauri.

Manspaa
KAMATI ya Fedha ya Baraza la Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma,limeshutumiwa na Madiwani wa Halmashauri hiyo kwa kujipendelea kupeleka fedha za miradi mingi ya maendeleo kwenye kata zao.
 
Madiwani hao walitoa kauli hiyo jana  wakati wakichangia taarifa ya Kamati hiyo ambayo ilionekana wajumbe wake wana miradi mingi ya maendeleo kuliko madiwani waliopo katika kamati nyingine na wakati huo huo kulikuwa na miradi mingine mipya ambayo ilikuwa imepangwa kufanyika katika kata zao.
 
Diwani wa Kata ya Kikombo Yona Kusaja (Chadema) alisema,fedha iliyopangwa kutekeleza miradi katika kipindi hiki zigawanywe kwa kata zote ili kuondoa sintofahamu hiyo.
 
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mbabala  Pascazia Mayala (CCM) alitaka Kamati hiyo ya fedha isipate fedha za kutekeleza mradi wowote mpaka kata nyingine zipate kwanza na kamati hiyo iwe ya mwisho.
 
Diwani wa Kata ya Msalato Ally Mohamed (CCM) ,katika Kata yake,wamejenga zahanati kwa kuwachangisha wananchi na jengo hilo limebaki sehemu ya chumba kimoja na nusu ,lakini Halmashauri imeshindwa kumpa fedha kidogo za kumalizia ujenzi wa jengo hilo na badala yake imekuwa ikitoa fedha kwa ajili ya miradi mipya katika kata zingine.
 
Hata hivyo baadhi ya wjumbe wa Kamati ya Fedha walionekana kukerwa na kauli za madiwani wenzao huku wakikanusha siyo kweli kwamba kamati hiyo imekuwa ikijipendelea kujipelekea fedha za miradi ya maendeleo.
 
Akichangia majadiliano hayo Diwani wa Kata ya Majengo Msinta Mayaoyao (CCM) alisema,siyo kweli kwamba miradi yote imeenda kwa wajumbe wa Kamati ya Fedha peke yao.
 
Diwani wa Kata ya Zuzu Awadhi Abdallah (CCM) alisema,yeye amekuwa Diwani kwa kipindi cha tatu lakini ndio amepata mradi kwa mara ya kwanza na hivyo siyo vyema kuwanyooshea vidole wajumbe wa Kamati yake.
Imeandaliwa na Barnaba Kisengi
#SIBUKAMEDIA

Comments

comments