Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN amewasili mjini LINDI.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN amewasili mjini LINDI mchana huu akitokea mkoa wa Dar es Salaam kwa njia ya barabara ambapo  kesho anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha   Sikukuu ya Wakulima Nanenane kitaifa kwenye viwanja wa NGONGO katika Manispaa ya LINDI.

Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN anatarajiwa kufunga maonyesho hayo ya Nane nane hapo kesho kwa  niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta JOHN POMBE MAGUFULI.

Alipowasili ikulu ndogo mjini LINDI, Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN  amepokelewa na Mkuu wa mkoa wa LINDI GODREY ZAMBI pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali na wa vyama vya siasa.

Katika Msafara wake, Makamu wa Rais ameambatana na Waziri wa Kilimo,Maliasili,mifugo na uvuvi wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  HAMAD RASHID.

  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments

Random Posts