Mafunzo ya wajasiriamali yamefanyika Chama cha Kuweka na kukopa TASWE-SACCOS

 TASWE

Ili kuendana na sera ya Tanzania ya viwanda ni vema kwa wajasiriamali kuhakikisha ubora wa bidhaa katika ushindani wa masoko ya kimataifa.

Akizungumza mwenyekiti wa chama cha kuweka na kukopa cha wajasiriamali wanawake Tanzania Bi. Anna Matinde ambaye  ni mmoja kati ya waandaaji wa mafunzo hayo amesema kuwa ili kuweza kujikwamua kiuchumi  ni vema kwa wajasiriamali hao kujua umuhimu wa mikopo na mchakato wake.

Ameongeza kuwa Taswe kwa kutambua hilo imetoa kipaumbele kwa wanawake katika kutetea maslahi yao ili kila mwanamke aweze kufurahi mafanikio katika Nyanja za biashara.

Nae meneja wa kanda ya NMB Benki  Bi Vicky Bishubo ambao ni waandaji walioshirikiana katika mafunzo hayo amesema kuwa kwa kutambua umuhimu wa  wadau wa biashara nchini wameona kuwa ni jambo la msingi kuwafahamisha umuhimu wa mikopo ambayo husaidia kukuza kipato na kujijenga kimaisha.

Fursa ya mafunzo kwa wajasiriamali yenye lengo la kuendeleza na kukuza uchumi ili  kuweza kukwamua jamii ipate maendeleo  imefanyika leo jijini Dar es salaam.

Wakati huohuo chama cha Taswe  na Remnant Generation Singers wamezindua albamu a kwaya inayoitwa “mbiu ya mgambo imelia sote tuondoke” .

Akizindua albamu hiyo mgeni rasmi mara baada ya kumalizika mafunzo hayo Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo,habari na utamaduni na sanaa Bw.Yusuph Singo ametoa pongezi kwa waimbaji hao kwa kuzindua albamu hiyo inayolenga jamii kuwa na maadili mema inayowafanya vijana kujitambua.

Aidha Bw. Singo amewaasa vijana kubadilika kwa kujituma katika kazi na kuachana na makundi yasiyo na maadili ili kuendana na nyakati husika za kukuza uchumi.

 

  • Mwandishi:
  • Tusse Kasambala.
  • SIBUKA MEDIA

Comments

comments