Maelfu ya watoto wa wakimbizi wa Burundi waanza shule nchini Rwanda

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) limetoa ripoti kuwa, maelfu ya watoto wa wakimbizi wa Burundi nchini Rwanda wameanza shule za nchi hiyo.

Tangu mwezi wa Julai mwaka jana, watoto wote wa Burundi wenye umri wa kwenda shule wameshirikishwa katika mpango wa miezi mitano unaolenga kuwawezesha wazoee mfumo wa elimu nchini Rwanda.

Katibu mkuu wa wizara inayoshughulikia maafa na wakimbizi Antoine Ruvebana amesema watoto wote wana haki ya kupata elimu. Pia amesema wanahitaji fedha na ushirikiano zaidi ili kuhakikisha kila mtoto anaweza kupata elimu.

Comments

comments