Mabaki ya meli ya abiria Athenia iliyozamishwa 1939 yagunduliwa baharini.

Nyambizi

Mabaki ya meli ya kwanza kuzamishwa wakati wa vita vya pili vya dunia yanaonekana kupatikana katika sakafu ya bahari ya Atlantic.

Mwindaji wa mabaki ya meli David Mearns, anasema inaonekana kuwa mabaki meli hiyo ya abiria ya Athenia huenda yapo mita 200 chini ya bahari nje ya pwani ya Ireland.

Nyambizi ya Ujerumani iliizamisha meli hiyo saa kadhaa baada ya Uingereza kutangaza vita dhidi ya Hitler mwaka 1939 ambapo zaidi ya watu 100 wengi raia wa Marekani waliuawa.

#SIBUKAMEDIA

 

 

Comments

comments