LAZARO NYALANDO atuma salamu za pole kwa Rais.

nyalandu.

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la SINGIDA KASKAZINI, LAZARO NYALANDU, , 2017 ametuma salamu za pole kwa Rais na Amri Jeshi Mkuu, DKT. JOHN POMBE MAGUFULI kufuatia vifo vya askari 14 wa JWTZ waliouawa nchini DR Congo walikokuwa wakilinda amani.

NYALANDU ametuma salamu zake za pole kwa familia za askari hao waliouwawa na wale waliojeruhiwa katika mapigano makali yaliyotokea nchini humo Disemba 7 na 8 kati ya askari wa Tanzania na Waasi wa Allied Democratic Forces (ADF) yaliyosababisha askari hao kupoteza maisha,kujeruhiwa na wengine kupotea.

Tayari miili  ya wanajeshi hao imewasili jijini DAR ES SALAAM kwa ndege maalum ya Umoja wa Mataifa, ambapo ilipelekwa kwenye Hospitali ya Jeshi LUGALO kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi ambapo Desemba 14 itaagwa.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, DKT. AUGUSTINE MAHIGA amewaambia waandishi wa habari kuwa  askari wote waliokuwa hawaonekani wamepatikana na uchunguzi unaendelea kwani inaonyesha mmoja wao kama alikuwa ameshikiliwa mateka.

#SIBUKAMEDIA

 

Comments

comments