Klabu ya soka ya Simba Kushiriki ligi kuu soka Tanzania Bara

simba

Klabu ya soka ya Simba inayoshiriki ligi kuu soka Tanzania Bara inataraji kushiriki katika mchezo wa kirafiki na timu ya soka ya polisi Dodoma inayoshiriki Ligi daraja la kwanza ikiwa ni maandalizi ya michezo mbalimbali inayoshiriki ikiwemo Ligi kuu pamoja na kombe la FA

Simba inayongoza katika msimamo wa ligi kuu soka Tanzania bara kwa kufikisha pointi 55 nyuma ya mahasimu wao Yanga ambao wana pointi 53, imewasili mkoani Dodoma ikiwa na wachezaji wote isipokuwa Method Mwanjari ambaye ni majeruhi ambapo mchezo huo wa kirafiki unataraji kupigwa katika Dimba la Jamhuri mjini Dodoma

Godfrey Nyange “Kaburu” ni makamu Mwenyekiti wa klabu ya Simba akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma amesema wachezaji wapo katika hali nzuri ya kutoa burudani kwa wakazi wa Dodoma na kuwataka mashabiki wa klabu hiyo wategemee soka safi

Naye Kocha wa timu ya Polisi Dodoma Paul Domishan alisema pamoja na kuwa Simba ni timu kubwa,amekiandaa kikosi chake vizuri kuhakikisha kinashinda katika mchezo huo unaosubiriwa na mashabiki wengi.

Katibu wa chama cha soka mkoani Dodoma Dorefa Hamis Kissoy ambao ndio wenyeji wa mchezo huo, alisema maandalizi ya mchezo huo yamekamilika na kuwataka waenzi wa soka mkoani hapa kujitokeza kupata burudani

Baada ya mchezo wa Simba na Polisi Dodoma kikosi cha Simba kitaondoka kuelekea Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma kucheza mechi ndogo ya kirafiki dhidi ya timu ya combine ya wilaya ya Chemba kabla ya kuelekea mkoani Arusha kukipiga na timu ya Madini katika kuwania kombe la FA

Mwandish: Barnaba Kisengi

#SIBUKA MEDIA

Comments

comments