Kiongozi wa upinzani Rwanda, atangaza serikali mbadala.

RWANDA

Kiongozi wa upinzani nchini Rwanda, ametangaza kuunda serikali sambamba na utawala uliopo Rwanda, lakini itakayokuwa ikifanya kazi nje ya nchi.

Thomas Nahimana ambaye ni kasisi wa zamani anayeishi nchini Ufaransa ametangaza kuunda serikali hiyo itakayofanyia kazi uhamishoni.

Katika mazungumzo na BBC, mwanasiasa huyo anasema lengo la serikali yake ni kuiondoa madarakani serikali ya rais Paul Kagame, anayemlaumu kuvunja sheria na kukandamiza wananchi.

Thomas Nahimana, amekatazwa kuingia Rwanda kujiandikisha kama mgombea wa kiti cha urais, katika uchaguzi mkuu unaopangiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu.

#SIBUKAMEDIA

#BBCSWAHILI

Comments

comments