Kenya kufunga kambi za wakimbizi za Kakuma na Dadaab

Serikali ya Kenya imetangaza kwamba itafunga kambi zote za wakimbizi nchini humo, hatua ambayo itaathiri wakimbizi wapatao 480, 000 wengi wakiwa wanatoka nchi jirani ya Somalia na Sudan Kusini.

Katibu wa kudumu katika wizara ya usalama wa kitaifa Karanja Kibicho amesema serikali inafunga kambi hizo kutokana na “mzigo mkubwa sana” wa kiusalama, kiuchumi na kimazingira.

Kibicho amesema idara ya kushughulikia wakimbizi nchini humo pia imefungwa kama hatua ya kwanza ya kufunga kambi hizo.

Comments

comments

Random Posts