Kemikali inayounda sehemu ya ndani ya dunia.

 

Utafiti unaonesha huenda silikoni ndiyo iliyochanganyikana na chuma na nikeli sehemu ya ndani kabisa ya dunia

Utafiti unaonesha huenda silikoni ndiyo iliyochanganyikana na chuma na nikeli sehemu ya ndani kabisa ya dunia

Wanasayansi nchini Japan wanasema wametambua kemikali ambayo inaunda sehemu ya ndani kabisa ya dunia.

Kemikali hiyo imekuwa ikitafutwa kwa miaka mingi, na inaaminika kuwa sehemu kubwa ya kitovu cha sayari ya dunia, baada ya madini ya chuma na nikeli.

Sasa, kwa kuunda mazingira yenye viwango vya juu sana vya joto na shinikizo sawa na ya sehemu ya ndani kabisa ya dunia, wanasayansi hao wamefanya utafiti ambao unaashiria huenda kemikali hiyo ni silikoni.

Ugunduzi huo huenda ukawasaidia wanasayansi katika kutambua ni jinsi gani dunia iliumbwa.

Mtafiti mkuu Eiji Ohtani, anayetoka chuo kikuu cha Tokyo ameambia BBC kwamba: “Tunaamini kwamba silicon ni sehemu kuu – karibu 5% (ya sehemu ya ndani kabisa ya dunia) kwa uzani huenda ikawa inajumuisha silicon ambayo imo ndani ya mchanganyiko wa chuma na nikeli.”

#Sibukamedia

#BBC SWAHILI

 

Comments

comments