Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo amesema wanaweza kumtumia wanavyotaka.

Katibu Mkuu wa  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),DKT.VICENT MASHINJI amesema chama hicho hakina ugomvi na aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la CHADEMA –BAVICHA ,PATROBAS KATAMBI na kwamba CCM wanaweza kumtumia wanavyotaka.

DKT.MASHINJI amesema hayo muda mfupi baada ya KATAMBI kutangazwa rasmi kuwa mwanachama wa CCM katika kikao cha Halmshauri Kuu ya CCM kinachoendela Ikulu jijini DAR ES SALAAM.

Amesema kama chama wameweka msimamo wao kuanzia ngazi ya udiwani kuwa mtu yeyote anaetaka kuhama chama ana uhuru wa kufanya hivyo wakati wowote ule.

Aidha DKT.MASHINJI ameongeza kuwa pamoja na kuwa walikuwa wamemuandaa KATAMBI kuja kuwa mwanasheria lakini kama ameamua hakuna sababu ya kumlazimisha abaki CHADEMA na kwamba wanamtakia kila la heri katika chama kipya alichoamua kujiunga.

PATROBAS KATAMBI ametangaza leo kujiunga na CCM katika mkutano wa Halmashauri Kuu-NEC uliofanyika Ikulu jijini DAR ES SALAAM.

  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments