Kampuni ya udalali ya YONO imefunga hoteli ya BLUE PEARL kwa kudaiwa kodi.

Kampuni ya udalali ya YONO imefunga hoteli ya BLUE PEARL  kwa kudaiwa kodi na mmiliki wa jengo alilopanga la UBUNGO PLAZA.

Kufuatia hatua hiyo hali ya sintofahamu imezuka majira ya asubuhi katika eneo hilo ambapo wageni waliokuwa wamelala hotelini hapo wasijue cha kufanya.

Akizungumza na waandishi wa habari hotelini hapo,Mkurugenzi wa YONO, SCOLASTICA KEVELA amesema hoteli hiyo inadaiwa kodi ya pango shilingi bilioni 5.7 na UBUNGO PLAZA.

SIBUKA FM ilifika eneo hilo asubuhi na kuzungumza na wateja ambao wengi wao wameonyeshwa kukerwa na hatua hiyo kwa madai kuwa wamepata usumbufu wengi wakiwa na familia zao.

  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments