Kampuni ya startimes Tanzania imeingia ubia na benki ya TPB.

UBIA.Still001

Kampuni ya startimes Tanzania imeingia ubia na benki ya TPB kwa lengo la kuwarahisishia wateja wake kupata huduma na television za kidigitali kupitia mkopo wa bei rahisi ambapo mteja atalazimika kulipa ndani ya miezi 12.

Akizungumza na sibuka fm Makamu wa rais wa startimes bi ZUHURA YUNUS  amesema ubia wa kibiashara walioingia na benki ya TPB utasaidia wateja wa startimes na wasio wateja   kupata huduma za kidigital kirahisi na kutimiza malengo yao kibiashara.

Aidha BI.ZUHURA ameongeza kuwa ushirikiano huo unaashiria mapinduzi ambayo benki na kampuni ya television zinaweza kuleta kwa kurahishia ulipaji wao na jamii yote.

UBIA.Still002

Naye Mkurugenzi wa benki ya TPB BW. JUMA MSUYA amesema watatoa ushirikiano mkubwa ili kuwapatia mkopo wateja wote kwa muda wa siku 3 bila usumbufu na wataanza na mashirika ya kiserikali na watu binafsi.

  • Mwandishi Amina Chekanae
  • Picha : Shyness Mdegela
  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments