Kampuni ya HALOTELI Imetoa Ufafanuzi wa tuhuma Zilizokuwa Zikiwakabili

jioneee zantel.Still002
Bw. Le Van Dai

Kampuni ya mawasiliano ya simu ya Halotel imetoa ufafanuzi kuhusu  tuhuma zilizokuwa  zikiikabili kampuni hiyo na kuisababishia serikali  hasara zaidi  ya  shilingi milioni 459 ambapo Halotel wamehusishwa na vipengele  viwili vya mashtaka.

Mashtaka hayo  ya Halotel ni  kushindwa kutoa taarifa ya  usajili wa kampuni ya mitambo ya UNEX Limited ambayo haikuwa kampuni iliyosajiliwa kikamilifu na TCRA  kwaajili ya kusajili line za simu 1000 zilizouzwa  kwa kampuni hiyo  pamoja na kushindwa kutimiza majukumu yao vizuri ya  kuuza  line za simu 1000.

Akizungumza mapema leo jijini Dar es salaam mkurugenzi wa Halotel Tanzania  Bw. Le Van Dai  amesema kampuni   imekana  kuhusika na makosa mengine ambayo yaliwahusisha watuhumiwa wengine ambao  ni wateja wa kampuni hiyo ikiwa ni pamoja na usimikwaji wa mitambo hiyo.

Bw. Christopher Masai
Bw. Christopher Masai

Amesema kuwa  kampuni hiyo  imekuwa ikiendesha  ikiendesha shughuli zake nchini  kwa kufata sheria na  taratibu zote   za mawasiliano ambazo zinatambuliwa na mamlaka  ya mawasiliano  Tanzania nchini (TCRA)

Naye Wakili wa Kampuni hiyo Bi Fatma Seif amesema kuwa  kwa mujibu wa mashtaka  yaliyosainiwa na mwendesha mashtaka mkuu wa serikali kuwa  terehe 16 mei 2017 ambayo inayotaja kampuni hiyo kuhusika na makosa hayo kifungu namba 6  na 7 ambavyo havihusishi kampuni hiyo na makosa ya washtakiwa wengine ambao sio wafanyakazi wa kampuni hiyo na  kuongeza kuwa  awana ushirikiano wowote na kampuni hiyo pamoja na raia hao wa Pakistani zaidi ya kuiuzia laini za simu kampuni hiyo baada ya kuwasilisha nyaraka zisizo halali.

Bi. Fatma Seif
Bi. Fatma Seif

“sisi  kama kampuni tunafanya kazi kwa usajili na vibali halali vya mamlaka husika  nchini na tumekuwa wawazi na kufata vibali kutoka mamlaka husika pamoja na kufata taratibu zote za kisheria “   alisisitiza Dai.

  • Mwandishi : Tuse Kasambala
  • #SIBUKAMEDIA

 

Comments

comments

Random Posts