Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii na Maendeleo imetembelea na kukagua miradi Chuo Kikuu.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii na Maendeleo  imetembelea na kuangalia miradi mbalimbali inayoendeshwa na kuratibiwa na Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM)

vlcsnap-2017-03-15-16h51m40s562

.Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa Mwenyekiti wa kamati hiyo Bw.Peter Serukamba amepongeza hatua iliyochukuliwa na chuo ya kuboresha na kukarabati baadhi ya miundombinu iliyodumu chuoni hapo kwa zaidi ya miaka 50.

Amesema hatua hiyo ya kuboresha na kuifanyia ukarabati miundombinu ni moja ya njia ya kuboresha mazingira ya utoaji mafunzo, taaluma kuwa bora zaidi hivyo kukiwezeaha chuo hicho kurudia hadhi yake ya kuwa moja ya chuo bora zaidi katika bara la afrika.

vlcsnap-2017-03-15-16h51m30s427

Nae Naibu waziri wa elimu, sayansi na teknolojia Mhandisi STELLA MANYANYA amesema serikali ya awamu ya tano imejikita zaidi katika kuhakikisha inatatua chongamoto zinazoikabili sekta ya elimu nchini kwa li kuwezesha wanafunzi kuwa na mazingira bora ya kujifunzia.

vlcsnap-2017-03-15-16h50m47s476

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es slaaam PROF  RWEKAZA MUKANDALA amesema changamoto kubwa iliyokuwepo chuoni hapo ni upungufu wa mabweni, maktaba pamoja na miundombinu.

Mwanahabari: Tuse Kasambala

#SIBUKAMEDIA

 

Comments

comments