Kamati iliyoundwa na Waziri wa Habari,vijana utamaduni sanaa na michezo NAPE NNAUYE.

NNAUYE

Kamati iliyoundwa na Waziri wa Habari,vijana utamaduni sanaa na michezo NAPE NNAUYE kwa ajili ya kuchunguza tukio la mkuu wa mkoa wa DAR ES SALAAM,PAUL MAKONDA kuvamia kituo cha kurushia matangazo cha clouds media umebaini kuwa mkuu huyo alivamia na kufanya vurugu kituoni hapo.

Aidha kamati hiyo imejiridhisha kweli kuwa mkuu huyo aliwatisha wafanyakazi wa kituo hicho kwa kuingia na askari na kuwatishia kuwataja kama watabisha kumtangazia kipindi chake.

Hayo yameelezwa leo jijini DAR ES SALAAM na Katibu wa kamati hiyo BW.DEODATUS BALILE wakati akitoa taarifa hiyo kwa waziri mwenye dhaman ya habari BW.NAPE NNAUYE.

Aidha kamati hiyo imemtaka mkuu wa mkoa wa DAR ES SALAAM,PAUL MAKONDA kuomba radhi wafanyakazi wa CLOUDS MEDIA kwa kitendo chake cha kuwavamia na askari kituoni hapo.

BALILE ameongeza kuwa kama kamati wamemuomba waziri awasilishe malalamiko kwa mamlaka ya uteuzi ichukue hatua zinazofaa ili kukomesha watawala wanaojisahau.a

Akizungumza baada ya kukanidhiwa ripoti hiyo waziri NAPE amewashukuru wajumbe wa kamati hiyo na kwamba ataipeleka kwa wahusika kwa ajili kuchukua hatua zaidi.

Hata hivyo amewataka wanahabari kuwa wavumilivu na kusisitiza kuwa Rais ana nia njema na tasnia ya habari hivyo ataendelea kushirikiana na wanahabari kwa kuwatia moyo na kuunga mkono waandishi wa habari

Mwandishi: Tuse Kasambala.

#SIBUAMEDIA

Comments

comments

Random Posts