Kamanda Mtui, ameelezea vifo vya ajali mkoani Kigoma.

treni kigoma

Mtu mmoja anaekadiriwa kuwa na umri wa miaka 30-35 mkazi  wa wilaya ya uvinza mkoani kigoma amefariki dunia papohapo  baada ya kugongwa na treni ya abiria iliyokuwa ikitokea mkoani Dodoma kuelekea mkoani kigoma.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi  mkoa wa kigoma naibu kamishina Ferdinand Mtui, amesema tukio hilo limetokea tarehe 6 June  mwaka huu katikati ya stesheni ya kalenge na kandaga ambapo marehemu alikuwa akitembea kwa mimiguu na kisha kuigonga treni hali iliyopelekea kifo chake.

Kamanda Mtui ameongeza kuwa mwili wa marehemu  umehifadhiwa katika hospitali ya mkoa wa Kigoma maweni kwa ajili ya uchunguzi pamoja na utambuzi kutoka kwa ndugu wa marehemu.

Aidha katika tukio lingine lililotokea June 8 mwaka huu  kamanada mtui amethibitisha kifo cha Idrisi Saadala mwenye umri wa miaka 65 mkulima na mkazi wa wilaya ya uvinza aliekutwa amefariki katika nyumba ya kulala wageni iitwayo new legeza mwendo  huku chanzo cha kifo chake kikiwa bado hakijajulikana.

Hata hivyo jeshi la polisi mkoani kigoma limetoa rai kwa wamiliki wa nyumba za kulala wageni kuwa na utaratibu wa kuwasijili wageni katika vitabu vya wageni kila wanapingia katika nyumba hizo.

  • Mwandishi : Saulo Steven
  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments

Random Posts