Jukwaa la katiba Tanzania (JUKATA) limebaini utekelezaji duni wa bajeti ya mwaka 2016/17 .

Jukwaa la katiba Tanzania (JUKATA) limebaini utekelezaji duni wa bajeti ya mwaka 2016/17 hasa ka tika miradi ya maendeleo ambapo serika liimepanga kutumia shilingi trilioni 29.5 kwa mwaka wa fedha 2016/17.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini  Dar es salaam mkurugenzi mtendaji wa jukwaa la katiba Bw. Hebron Mwakagenda    a mesema katika bajeti ya serikali kwa miradi ya maendeleo kwa mwaka unaoelekea mwishoni ilikuwa ni trilioni 11.8 sawa na asilimia 40 ya bajeti kuu ambapo hadi kufikia mwezi march mwaka 2017 miezi mitatu kabla ya utekelezaji wa bajeti kukamilika imepeleka shilingi trilioni 3.5 tu ambayo ni sawa na asilimia 34 ya fedha zilizopangwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Mwakagenda amesema kufuatia mwenendo huo hafifu wa utekelezaji wabajeti umetoa   cha asilimia 50 hadi kufikia mwisho wa mwaka bajeti ambao ni mwezi Julai hivyo kupeleka bajeti ya mwaka 2017/18 yenye mwendelezo kama huo kukosa kutotekelezeka hivyo kufanya azma ya viwanda kushindwa kufikiwa.

Bw. Mwakagenda ametoa pongezi kwa Profesa Palamagamba Kabudi kwa kuteuliwa kuwa waziri wa katiba na sheria kwa kuwaa nao ujuzi katika kuongoza wizara hiyo  muhimu pamoja na ushiriki wake akiwa kamishna watume ya mabadiliko ya katiba mpya hivo amepitia uzoefu ambao utasaidia katika kuelekea mchakato wa katiba mpyaa mbao haupo bayana.

Aidha jukwaa la katiba limepokea mtazamo chanya kuhusu taarifa kwamba serikali ya awamu ya tano ina mpango wa kuendeleana mchakato wa kuandika katiba mpya kwa mujibu wa kauli ya waziri wa katiba na sheria profesa Kabudia liyoitoa kwa wa bunge wa kamati ya bunge ya kudumu ya katiba na sharia kwamba serikali natarajia kuanza marekebisho ya sheria ilikua kamilisha mchakato huo.

Amezitaja changamoto kuu mbili  ambazo zinahitaji kupatiwa ufumbuzi katika kuelekea mchakato wa katiba kuwani sharia ya mabadiliko ya katiba namba nane ya mwaka 2011 na sharia ya kura ya maoni ya mwaka 2013.

Imeadaliwa na Tuse Kasamala.

#SIBUKAMEDIA

 

Comments

comments