Jordan yaionya Marekani ikiitaka isiutambue Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.

REX

Ayman Safadi alisema alimuambia waziri wa mashauri wa nchi za kigeni wa Marekani Rex Tillerson kuwa hatua kama hiyo inaweza kuzua ghadhabu kubwa kwa nchi za kiarabu na ulimwengu wa kiisalmu.

Kuna uvumi kuwa Rais Donald Trump atatangaza hilo hivi karibuni na kutimiza ahadi yake aliyotoa wakati wa kampeni.

Jared Kushner, mkwe wa Trump alisema kuwa bado hakuna uamuzi uliofanywa

Katika mtandao wa Twitter, Bw Safadi alisema: #Nilizungumza na waziri Rex Tillerson kuhusu hatari ya kuutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel. Hatua kama hiyo inaweza kusababisha ghadhabu kwenye nchi za kiarabu na kwa ulimwengi wa kiislamu na kuzua misukosuko na pia kuhujumu jitihada za amani.”

#SIBUKAMEDIA.

Comments

comments