Jiwe kubwa sana kupita karibu na dunia.

Jiwe Kubwa

Jiwe kubwa zaidi kuwahi kupita karibu na dunia katika kipindi cha karibu karne moja linatarajiwa kupita karibu na sayari ya dunia umbali wa karibu maili milioni 4.4 , kimesema kituo cha masuala ya anga za juu cha Marekani, Nasa.

Vipimo vya Florence vilikadiria umbali wa maili 2.7 sawa na kipenyo cha 4.4 na kwamba jiwe hilo halina tisho kwa dunia kwa karne zijazo

Mawe mengine yaliyowahi kupita karibu na dunia, yalikadiriwa kuwa ni madogo sana.

Mawe hayo ambayo yana umbo la vifusi upande wa kushoto ni masalia yaliyobaki wakati wakuundwa kwa jua na sayari.

Jiwe la Florence – lililogundulika mnamo mwaka 1981- linaweza kuwa mara 18 ya wastani wa umbali baina ya dunia na mwezi.

“Florence ni jiwe kubwa zaidi kuwahi kupita karibu na dunia yetu tangu kuanzishwa kwa mpango wa shirika la anga za mbali la Marekani NASA wa kuchunguza na kubaini mawe yaliyopo karibu na dunia ,” Amesema Paul Chodas, meneja wa kituo cha NASA kinachochunguza vitu vilivyopo karibu na dunia katika taarifa yake.

  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments