Jeshi la Polisi mkoani DODOMA limeyataka makampuni ya Ulinzi mkoani DODOMA kuacha tabia ya kuazimisha silaha kwa watu wengine

Silaha

Jeshi la Polisi mkoani DODOMA limeyataka makampuni ya Ulinzi mkoani DODOMA kuacha tabia ya kuazimisha silaha kwa watu wengine ili kuhakikisha wanatunza usalama wa silaha hizo ikiwemo matumizi mabovu.

Hayo yamesemwa na Mrakibu Mwandamizi wa Polisi mkoa wa DODOMA, DAVID MAFWINDA, kwa Niaba ya Kamanda wa Polisi mkoa,katika mkutano wa makampuni ya Ulinzi.

Kamanda MAFWINDA amesema kuwa hakuna kosa kubwa kama la kuazimisha silaha, kwa sababu asiyemmliki anaweza kwenda kuitumia katika matumizi ambayo siyo sahihi.

Kutokana na hilo kamanda huyo ametoa onyo hilo kwa makampuni yenye tabia ya kuazimisha silaha kwa watu wengine, na kuwataka wafuate sheria za umiliki wa silaha.

Naye Mwenyekiti wa Sekta ya Walinzi nchini FELIX KAGISA amesema lengo la mkutano huo ni pamoja na kuweka mikakati ya kuhakikisha wanaboresha sekta hiyo ili walinzi wafanye kazi kwa amani na usalama.

Aidha amesema moja ya mikakati ambayo wamejiwekea ni kuhakikisha walinzi wote wanakuwa na leseni ya kufanya kazi, ikiwamo kufuatilia sheria ya kuwalinda wakiwa kazini.

Hata hivyo amesema wanatarajia kutoa mafunzo kwa raia ili wanapoajiriwa katika kazi hizo wawe na uwezo wa kuzifanya.

#SIBUKAMEDIA

Comments

comments