JESHI la Polisi mkoa wa SIMIYU limeshauriwa kuwapiga marufuku wapiga debe katika vituo vyote vya kusafirisha abiria vilivyopo mkoani.

Wapiga Debe

JESHI la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa SIMIYU limeshauriwa kuwapiga marufuku wapiga debe katika vituo vyote vya kusafirisha abiria vilivyopo mkoani kutokana na kusumbuliwa kwa abiria na wengine kuibiwa mizigo yao na wapiga debe hao.

Pia wamelitaka jeshi hilo kuwadhibiti madereva wote wanaojaza abiria kupita kiasi sambamba na kuwachukulia hatua za kinidhamu askari wa kikosi hicho wanaoshindwa kuwakamata madereva wanaofanya vitendo hivyo kwa kuwa  vinahatarisha usalama wa abiria wao.

Wakizungumza na Waandishi wa habari mjini BARIADI baadhi ya abiria hao wamesema kuwa wamekuwa wakifanyiwa fujo na wapiga debe hao pindi wanapofika katika stendi ya mabasi ya mjini BARIADI.

Wamesema kuwa sasa ifike wakati kwa jeshi la polisi kuendesha oparesheni maalum ya kuwaondoa wapiga debe katika vituo vyote vya kusafirishia abiria katika mkoa wa Simiyu hadi maeneo ya stendi zawilayani.

Pia wameliomba jeshi hilo kuwabadilishia majukumu askari wa usalama barabarani ambao wamekuwa kila mara wakilalamikiwa kutokana na kujihusisha na vitendo vya rushwa.

#SIBUKAMEDIA

Comments

comments