Jeshi la Polisi linatoa rai kwa wananchi kuacha kutumia mitandao ya kijamii vibaya na badala yake mitandao hii itumike kwa ajili ya kuelimisha na kuihabarisha jamii

Social media

Jeshi la Polisi linatoa rai kwa wananchi kuacha kutumia mitandao ya kijamii vibaya na badala yake mitandao hii itumike kwa ajili ya kuelimisha na kuihabarisha jamii juu ya masuala mbalimbali ya kimaendeleo.

Wito huo umetolewa na msemaji wa polisi  Makao Makuu BW.DAVID MWAKALUKWA  jijini DAR ES SALAAM  kufuatia baadhi ya watu kutumia majina na picha za watu na kuwahusisha na matukio ya kihalifu kitendo ambacho ni kinyume na sheria.

Amesema tarehe 11.09.2017 kupitia mitandao ya kijamii kulisambaa picha ya askari wa Jeshi la Polisi akihusishwa na muendelezo wa tukio la kujeruhiwa kwa risasi kwa Mbunge wa SINGIDA MASHARIKI TUNDU LISSU (MB) ambapo taarifa hiyo ilimtambulisha askari huyo kuwa ni kachero wa Kitengo cha Interpol na kwamba yupo jijini NAIROBI nchini KENYA akifuatilia taarifa za mbunge huyo.

Jeshi la Polisi linapenda kukanusha taarifa hizo kuwa si za kweli na ni za uongo zenye lengo la kumchafua askari huyo na Jeshi la Polisi kwa ujumla na kusisitiza kuwa  Askari huyo hayupo NAIROBI kama ilivyoenezwa na picha iliyotumika ilipigwa hapa nchini tarehe 07.01.2017 kwenye sherehe ya mahafali ya mtoto wa kaka yake. 

Jeshi la Polisi linakemea vikali kitendo hiki na linawataka wale wote waliohusika kusambaza au kutajwa katika taarifa hizo kuripoti kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kwa ajili ya mahojiano.

Kuhusu suala la LISSU  amesema lipo chini ya uchunguzi ili kuwabaini wote waliohusika na tukio hili na hatimaye kuwafikisha mahakamani na kuwaomba wananchi  na wanasiasa kuliachia Jeshi la Polisi liweze kufanya kazi yake bila kuliingilia ili kuweza kupata ukweli wa jambo hili .

  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments