Jeshi la Polisi limewatoa hofu wakazi wa Dar es salaam

Jeshi la polisi kanda maalum ya DAR ES SALAAM limewatoa hofu wakazi wa jiji hili na kusema kuwa hali ni shwari wakati huu wa kuelekea sikukuu ya mwaka mpay.
 
Aidha jeshi la polisi limewataka wakazi wa jiji hili kufuata maelekezo ya namna ya kufyatua risasi na fataki wakati wa sherehe za mwaka mpya kwa kuwakutanisha wakazi wa jiji katika viwanja vya Tanganyika Packers ,kawe jijini DAR ES SALAAM.
 
Hayo yameelezwa leo jijini DAR ES SALAAM na kamishina wa polisi kanda maalum ya DAR ES SALAAM, LAZARO MAMBOSASA wakati akitoa tahimini ya matukio ya mwaka 2017.
 
Kamanda MAMBOSASA amewaambia waandishi wa habari kuwa matukio ya uvunjifu wa amani yamepungua katika jiji la DAR ES SALAAM ukilinganisha na mwaka uliopita.
 
Aidha kamanda MAMBOSASA amewasihi wakazi wa jiji kuacha kutumia silaha hovyo,kuvuta bangi na aina nyingine zote za uhalifu kwa kuwa jeshi la polisi liko makini na litawakamata watakaokiuka maagizo hayo.
 
Akizungumzia suala la kukamatwa kwa Kiongozi wa kiroho askofu ZAKARIA KAKOBE ,MAMBOSASA amesema jeshi la polisi halijamkamata na pale itakapohitajika atakamatwa lakini kwa sasa hajakamatwa.
#Sibukamedia

Comments

comments

Random Posts