Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam linawashikilia watu wawili madereva bodaboda kwa kosa la kujihusisha na matukio ya ujambazi.

CIRRO

Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam linawashikilia watu wawili madereva bodaboda kwa kosa la kujihusisha na matukio ya ujambazi pamoja na uporaji.

Kamanda wa polisi kanda maalum  ya Dar es salaam CP SIRRO amewataja watuhumiwa hao ni Mathias Nathan mwendesha bodaboda mkazi wa Kawe.

Amesema jeshi la polisi baada ya kupata taarifa zinazomhusisha mtuhumiwa huyo na mauaji lilianza kumfatilia tangu tarehe 2 ya mwezi wa kwanza 2012 ambako tukio hilo lilitokea huko Boko Basihaya ambako mlinzi wa grosari aliuwawa  kwa kupigwa risasi kichwani na majambazi na kupora pesa taslimu shilingi milioni 1.3.

Kamanda Sirro ameongeza kuwa baada ya mahojiano na mtuhumiwa huyo alikiri kuhusika na tukio hilo na kumtaja mwenzake Martini Daud mwenye umri wa miaka 36 ambaye ni mkazi wa Boko njiapanda ya magereza.

Baada ya jeshi la polisi kufanya upekuzi nyumbani kwake walifanikiwa kukamata silaha moja aina ya bunduki Shortgun Pump Action yenye namba D.918884 TZCAR  76475.

Kamanda Sirro Ameongeza kuwa majambazi hao walikuwa wakimili bunduki ambayo waliificha katika maeneo ya Ununio katika mabwawa ya Chumvi pembezoni mwa bahari ya Hindi.

Imeandaliwa na Tuse Kasambala

#SIBUKAMEDIA

Comments

comments