Jengo la wizara ya Maji limeanza Kubomolewa.

Jengo la Wizara ya Maji na Umwagiliaji lililo ndani ya hifadhi ya Barabara ya Morogoro jijini Dar es Salaam limeanza kubomolewa rasmi kupisha ujenzi wa barabara za juu.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,DKT.JOHN POMBE alilolitoa novemba 15,2017 kwa uongozi wa wizara hiyo, na ghorofa la Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuwekwa alama ya X na kubomolewa kupisha upanuzi wa barabara hiyo.

Radio SIBUKA FM imeshuhudia tingatinga likivunja ukuta katika ofisi ya waziri  wa maji huku watu wengine wakiendelea na kazi ya kuondoa madirisha na milango kwenye majengo.

Aidha TANROADS inaendelea kuweka alama X kwenye nyumba za wananchi zilizo ndani ya hifadhi ya barabara  kuanzia eneo hilo la UBUNGO mpaka KIMARA MWISHO.

Kwa mujibu wa Tanroads, ubomoaji katika eneo la UBUNGO hadi KIMARA MWISHO unahusisha nyumba zilizo mita 91.7 katika hifadhi ya barabara ikiwa ni utekelezaji wa Sheria ya Hifadhi ya Barabara ya mwaka 1932.

 #SIBUKAMEDIA

 

 

 

 

 

 

Comments

comments