Jamii imeshauriwa kuwapa watoto wa kike lishe bora tangu utotoni.

lishe bora

Jamii imeshauriwa kuwapa watoto wa kike lishe bora tangu utotoni ili kuwasaidia kujenga nyonga   bora ambazo zitawasaidia kujifungua salama pindi watakapokuwa watu wazima.

Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Dr.James Chopa kutoka CCRBT katika  mafunzo ya waandishi wa habari yaliyoandaliwa na shirika la umoja wa mataifa la idadi ya watu (UNFPA) na wadau wa afya ya siku ya kimataifa katika kuhakikisha fistula inatokomezwa duniani kuwa matunzo ya lishe borautotoni ni muhimu katika kuepuka fistula ukubwani.

Aidha amezitaja sababu kuu  zinazosababisha fistula kuwa ni uchungu pingamizi ,ucheleweshwaji wakati wa kujifungua na kubainisha tatizo hili limekuwa likiikumba nchi zinazoendelea zaidi.

Nae Bi.Martha Rimoyi kutoka chama cha wakunga Tanzania amewaasa waandishi kusaidia kuelimisha jamii  ili kupunguza vifo vya wanawake wajawazito ambavyo vimeongezeka kutoka 454 hadi kufikia 556 kwa kila vizazi hai laki moja.

Kilele cha maadhimisho ya siku ya fistula duniani ni tarehe 23 mwezi mei 2017.

  • Mwandishi : Tuse Kasambala
  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments