Iwobi: Wenger ni muhimu sana kwetu

Wenger

Mshambuliaji wa Arsenal Alex Iwobi anataka meneja wa klabu hiyo Arsene Wenger kusalia Emirates na kusema kuwa kukosolewa kwake sio sahihi.

Wenger mwenye umri wa miaka 67 amekuwa akikosolewa na mashabiki wa timu hiyo baada ya timu yake kushuka mpaka nafasi ya sita katika msimamo wa ligi ya EPL kufuatia kufungwa katika michezo mitano iliyopita.

Magoli 10-2 ikiwa ni uwiano waliofungwa na Bayern Munich katika michuano ya Ulaya imeongeza msukumo kwa meneja huyo, huku akisema kuwa atafanya maamuzi sahihi katika siku za usoni.

Ni mtu sahihi kwa mawazo yangu,” alisema Iwobi mwenye miaka 20.”Ningelipenda yeye abakie.”

Mkataba wa Wenger unamalizika mwishoni mwa msimu huu, lakini amepewa ofa ya kuongeza miaka miwili.

#SIBUKAMEDIA

#BBC SWAHILI

Comments

comments