Itel mobile mapema leo imeungana na watoto wenye mahitaji maalum kuonyesha upendo


IMG-20170623-WA0007

Itel mobile mapema leo imeungana na watoto wenye mahitaji maalum kwa kuonyesha upendo katika kuelekea msimu wa sikukuu za Eid Al Fitr.

IMG-20170623-WA0006

Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es salaam na kuwakilishwa vema na balozi wa Itel Irene Uwoya ambapo wamejumuika na watoto yatima wa kituo cha CHAKUWAMA na kutoa zawadi mbalimbali.

Akizungumza mkurugenzi wa Itel Bw.Saimon Asajile amesema kuwa wanaunga mkono jitihada zinazofanywa na kituo hicho cha kulelea watoto yatima na vinginevyo kwa kuhakikisha watoto wanakuwa na furaha na kupata mahitaji wanayostahili.

IMG-20170623-WA0021

Kwa upande wake katibu mtendaji wa kituo hicho Bw.Hassan Khamis ametoa shukrani kwa Itel mobile na balozi wake kwa kuwakumbuka watoto hao kwa mahitaji muhimu.

IMG-20170623-WA0010

Aidha amebainisha changamoto zinazowakabili watoto ni katika matibabu ya afya na kuiomba jamii iendelee kuweka ushirikiano ili kuwapa faraja watoto yatima.

IMG-20170623-WA0020

Nae meneja masoko Bw.Wolle Fernand ametoa wito kwa jamii kuungana na Itel mobile Tanzania kuonesha upendo kwa kununua bidhaa hizo kwakuwa kufanya hivo watakuwa wamechangia makundi hayo maalum ya jamii yenye uhitaji.

Mwandishi :Tuse Kasambala

#SIBUKAMEDIA

Comments

comments