Idadi ya mauzo ya hati fungani imeongezeka mara tatu.

img-20161227-wa0016

Patrick msusa Meneja Miradi

Idadi ya mauzo ya hati fungani imeongezeka mara tatu zaidi ya mauzo ya wiki iliyopita katika soko la hisa na kufikia shilingi za kitanzania bilioni 22 ambapo hati fungani 8 ziliingia sokoni wiki hii tofauti na wiki iliyopita hati fungani moja tu iliingia sokoni.

Akizungumza na waandishi wa habari meneja mradi na biashara wa soko la hisa Dar es salaam Bw.Patrick msusa Amesema kuwa hesabu za robo ya mwisho mwaka huu kuwa jumla ya matzo ya mwezi octoba hadi desemba 2016yamefikia bilioni 102 ambapo ni ongezeko la 6% kuzidi idadi ya mauzo ya robo ya mwisho wa mwaka 2015 ambayo jumla yamefikia shilingi bilioni 92.

Meneja msusa amesema kuwa idadi ya mauzo ya hisa wiki hii yamepungua kwa 32% pamoja na idadi ya hisa imepungua kwa 25% na kuwa punguzo hilo linaashiria kupungua Xmas na mwaka mpya kutokana na fedha nyingi kuelekezwa katika shughuli za kijamii.

Aidha amesema kuwa umma unajiandaa na mauzo ya hisa za makampuni ya simu ambayo yanatarajiwa kuanza hapo mwakani na kusema kuwa kampuni zilizoongoza kwa idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa ni TBL kwa 66.5%,CRDB bank kwa 16%na MKCB bank kwa 8.3%.
Hatahivyo amesema kuwa ukubwa wa mtaji wa makampuni kwa jumla ulipanda kwa 1.1% hadi kufikia trillion 19.6 ambapo makampuni ya ndani umeendelea kubaki kwenye kiwango cha trilioni 7.7 .

Wiki hadi wiki ambapo viashiria sekta ya viwanda imebaki kwenye wastani wa shiliingi za kitanzania 4,665 wiki hadi wiki ambapo sekta ya huduma za kibenki na fedha Imeshuka kwa pointi 5.

Kutokana na punguzo la bei ya hisa za DSE kwa asilimia 15.25 ambapo DSE Ilikuwa kampuni ya pili iliyopata punguzo kubwa la hisa zake sokoni baada ya NMG ambapo ilipata punguzo la 27.18%

#SIBUKAMEDIA

#Imeandaliwa na Tuse Kasambala

Comments

comments