Hospital ya Aga Khan Yazindua Kituo Kipya Cha Huduma Mikocheni

Wamiliki wa hospitali na vituo vya afya vya binafsi kote nchini wamepongezwa kwa kuendelea kusogeza huduma za matibabu karibu zaidi na wananchi katika kuunga mkono juhudi za serikali za kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma bora na salama.

vlcsnap-2017-02-28-05h57m53s71 

Pongezi hizo zimetolewa mapema leo jijini Dar-es-Salaam na Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni DR.Aziz Msuya wakati akizindua kituo kipya cha kutolea huduma kilichojengwa na hospitali ya Aga Khan na kuongeza kuwa hospitali hiyo inahitaji kuungwa mkono katika jitihada inazofanya za kuhakikisha mtanzania anapata matibabu yanayostahili na kwa wakati.

vlcsnap-2017-02-28-05h57m00s60

 Dr.Msuya ameongeza kuwa serikali itakuwa tayari wakati wote kutoa ushauri pale inapobidi kwa hospitali hiyo ikiwa ni pamoja na kuipatia chanjo ya magonjwa mbalimbali pale itakapohitajika,sambamba na hilo ameuomba uongozi wa hospitali hiyo kuendelea kuchoma taka sehemu inayohusika ili kuendelea kuenzi na kutunza mazingira.

Imeandaliwa na Stanley Burushi

#SIBUKAMEDIA

 Naye muuguzi mkuu wa hospitali ya Aga Khan Bi.Lucy Kway amewakumbusha watanzania kuwa hospitali hiyo hutoa huduma ya bure ya uchunguzi wa saratani

Comments

comments