Hamisi Shilla miaka 30, akikabiliwa na mashtaka mawili ya kubaka.

SINGIDA

Mtu mmoja mkazi wa kijiji cha Mampanta kata ya Old- Kiomboi wilayani Iramba mkoa wa Singida aliyefahamika kwa jina la Hamisi Shilla miaka 30, amefikishwa katika  mahakama ya wilaya ya Iramba akikabiliwa na mashtaka mawili ya kubaka.

Mwendesha mastaka wa polisi kwa niaba ya jamuhuri mkaguzi msaidizi,  Salumu Ally Nannume, amesema mshtakiwa huyo ametenda makosa hayo  kinyume na kifungu cha 130 {1}{e} na kifungu cha  131 cha kanuni ya adhabu sura  ya 16 marejeo ya mwaka 2002.

Nannume ameeleza kuwa mshtakiwa Hamisi Shilla anashtakiwa mnamo agosti 06 mwaka huu majira ya saa kumi alasiri huko katika kijiji cha Mampanta amewabaka watoto wawili kwa wakati mmoja.

Imeelezwa kuwa majira hayo mshtakiwa amembaka binti mwenye umri wa miaka 12; na baadaye tena  kumbaka binti wa miaka 11, huku akijua kufanya hivyo ni kinyume na katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania hata hivyo Kesi hiyo itatajwa tena Agusti 21 mwaka huu.

  • Mwandishi : Saulo Stephen.
  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments

Random Posts