Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi leo imewapokea na kuwarudisha katika chama hicho wanachama kadhaa kutoka vyama vya upinzani.

CCM

Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) inaendelea na vikao vyake Ikulu jijini DAR ES SALAAM, ambapo leo imewapokea na kuwarudisha katika chama hicho wanachama kadhaa kutoka vyama vya upinzani ambao walijitokeza kuomba kujiunga na chama hicho.

Miongoni mwa wanachama walipokolewa ni PROFESA KITILA MKUMBO, SAMSON MWIGAMBA, EDNA SUNGA (wote kutoka ACT-Wazalendo) (kutoka ACT-Wazalendo), LAWRENCE MASHA na PATROBAS KITAMBI (Chadema).

Akizungumza baada ya kuwapokea Mwenyekiti wa CCM Taifa, DKT.JOHN POMBE MAGUFULI amewapongeza kwa kujiunga CCM na kuongeza kuwa hatua yao ya kujiunga na CCM hicho isije ikawa majaribio bali wahakikishe uamuzi wao huo uwe wa kudumu.

Hata hivyo, Rais DKT. MAGUFULI amewapa ruhusa ya kugombea nyadhifa mbalinmbali ndani ya chama na kwenye maeneo yao ili kuimarisha demokrasia ndani ya chama hicho..

 

Akizungumza baada ya kukaribishwa  PATROBAS KATAMBI amesema amejiunga CCM si kwa sababu ya madaraka bali kwa ajili ya maslahi ya Taifa na kusisitiza kuwa yuko tayari kuitwa msaliti kwa kusaliti ubinafsi na kundi la wabinafsi.

Hata hivyo, KATAMBI amesema kuwa ameona CCM inawapatia vijana nafasi na fursa za kuongoza tofauti na alipotoka kwamba vijana wakishatumiwa wanaonekana kama takataka yaani ni kama karai baada ya ujenzi.

Wakati huo huo Kada wa zamani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), SOFIA SIMBA amerejeshwa ndani ya chama hicho miezi kadhaa baada ya kufukuzwa kwa usaliti.

Mama Simba ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake -CCM (UWC), amerejeshwa baada ya kuomba msamaha.

Uamuzi huo umefikiwa leo katika Mkutano wa Kamati Kuu (NEC-CCM), baada ya Mwenyekiti wa chama hicho, Rais DKT.JOHN MAGUFULI kusoma barua yake ya kuomba msamaha na kuwahoji wajumbe wa kikao hicho.

SOFIA SIMBA alifukuzwa uanachama na kikao cha NEC baada ya vuguvugu la Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, baada ya kukutwa na hatia za kuwa msaliti kwa kuwasiliana na kambi ya mgombea urais wa CHADEMA, EDWARD LOWASSA wakati wa kampeni.

#SIBUKAMEDIA

 

Comments

comments