Halmashauri kuanza ujenzi wa ofisi za serikali za mitaa.

seleman jaffo

Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)  SELEMAN JAFFO ametoa muda wa mwezi mmoja na nusu  kwa halmashauri ambazo hazijaanza ujenzi wa ofisi zao  licha ya serikali kutoa fedha kwa ajili wa ujenzi huo  zitanyang”anywa fedha hizo na kupewa halmashauri nyingine

Naibu Waziri JAFFO amefika katika eneo la ujenzi wa ofisi ya halmashauri ya wilaya ya CHAMWINO katika manispaa ya DODOMA na kuridhika na hatua ya ujenzi huo na kutoa onyo kwa baadhi ya halmashauri ambazo hazijaanza ujenzi wa ofisi zao kuwa watanyanganya fedha.

Mradi huu wa  ujenzi unajengwa na SUMA JKT ambao wameahidi kukamilisha sehemu ya chini  ya jengo hilo ndani ya miezi minne.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya CHAMWINO ATHUMAN MASASI amesema kukamilika wa ofisi hizo itasaidia ufanisi wa kazi kwa watumishi wa halmashauri hiyo na kuweza kuwatumikia wananchi kwa wakati.

Naibu Waziri JAFFO ameagiza kukamilika mapema kwa ujenzi huo na kuanza kutumika kwa ofisi hizo kuanzia january mosi  mwaka 2018, huku  Ujenzi huo ukigharimu zaidi ya shilingi milion miasaba  kwa sehemu ya chini  ya jengo hilo.

  • #SIBUKAMEDIA

Comments

comments