HALI YA SINTOFAHAMU IMEENDELEA KUJITOKEZA KWA WAFANYABIASHARA WA SOKO LA SARAFINA.

HALI YA SINTOFAHAMU IMEENDELEA KUJITOKEZA KWA WAFANYABIASHARA WA SOKO LA SARAFINA LILILOPO  MANISPAA YA DODOMA KUTAKIWA KUSAINI MIKATABA NA KAMPUNI HODHI YA RASILIMALI ZA RELI (RAHCO) YA WAO KUENDELEA KUWEPO MAHALI HAPO ILI HALI SERIKALI YA MKOA ILIKWISHA WATAKA KUTOKUFANYA HIVYO.

WAKIONGEA NA SIBUKA MAISHA FM

WAFANYABIASHARA HAO WAMESEMA KUWA HADI SASA WAKO NJIA PANDA KUTOKANA NA KAULI ZA PANDE ZOTE MBILI KWANI AWALI WALIAMBIWA KUWA WASISAINI MIKATABA HIYO NA KUWA WANATAFUTIWA MAENEO YA KUPELEKWA.

KWA UPANDE WAKE MKURUGENZI WA MANISPAA YA DODOMA BW.GODWIN KUNAMBI AMEIAMBIA SIBUKA MAISHA FM KUWA NAYE ANASHANGAZWA NA HALI HIYO KWANI TAYARI WALIKWISHA FANYA MAZUNGUMZO BAINA YA UONGOZI WA RAHCO,MANISPAA PAMOJA NA MKUU WA MKOA KISHA KUWA NA MAKUBALIANO YA PAMOJA.

PIA SIBUKA MAISHA FM IMEMTAFUTA MKURUGENZI WA RAHCO BW.MASANJA KADOGOO AMBAYE AMESEMA KUWA MAENEO HAYO NI YA RELI HIVYO NI LAZIMA  UTARATIBU UFUATWE.

HATA HIVYO MKUU WA MKOA WA DODOMA MH.JORDAN RUGIMBANA AMESEMA KUWA  KWA SASA KAMA MKOA WANAFANYA UTARATIBU WA KUWAHAMISHA WAFANYABIASHARA HAO NA WATATOA TAARIFA RASMI WIKI IJAYO JUU YA SINTOFAHAMU ILIYOPO KWA SASA.

Imeandaliwa na Barnabas Kisengi

#SIBUKAMEDIA

 

Comments

comments