Hali ya mbunge wa Singida yazidi kuimarika.

LISUu

Hali ya mbunge wa SINGIDA MASHARIKI ,TUNDU LISSU inazidi kuimarika ambapo taarifa kutoka jijini NAIROBI zinasema ameanza kukaa bila msaada.

TUNDU LISSU ambaye anaendelea na matibabu,leo ameweza kuinuka na kukaa baada ya kulala kitandani bila kuinuka kwa zaidi ya miezi mitatu.

Akiwa hospitalini hapo LISSU anaonekana mwenye matumaini hasa baada ya wiki hii kuzungumza na chombo kimoja cha habari na kukiri kuwa hana majeraha,anaendelea vizuri licha ya kuwa ana risasi moja mwilini

Mbunge huyo ambae pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika alivamiwa na watu wasiojulikana Agosti 8,mwaka huu na kupigwa risasi zaidi ya 30 akiwa njiani kuelekea nyumbani kwake area D huko mkoani DODOMA.

Comments

comments