Hali ya kisiasa nchini Kenya yadhuru sekta ya utalii

Wadau wa sekta ya utalii nchini Kenya jana walisema hali ya sasa ya kisiasa nchini Kenya itawatisha watalii na watu wanaotaka kuwekeza nchini Kenya.

Waziri wa utalii wa Kenya Bw. Najib Balala amesema maandamano dhidi ya tume ya uchaguzi yanayofanywa na makundi ya upinzani yanaiathiri sekta ya utalii.

Bw. Balala ametahadharisha kuwa Kenya itaathiriwa na ukosefu wa ajira, na tayari sekta ya utalii imeanza kuathirika, na kama hali haitabadilika hali ya sekta ya utalii itazidi kuwa mbaya.

Sekta ya utalii imekuwa inafufuka tangu mwezi Novemba mwaka jana baada ya meli za watalii kuwasili kwenye bandari ya Mombasa.

Comments

comments