Emmanuel Macron ashinda uchaguzi wa urais Ufaransa.

3

Emmanuel Macron ameshinda Uchaguzi wa Urais wa Ufaransa. Matokeo yanaonesha Macron amemuacha kwa mbali mpinzani wake Bi Marine Le Pen kwa kujinyakulia asilimia 65 ya kura.

Maelfu ya wanaomuunga mkono Macron walisherehekea katika kati mwa Paris wakipeperusha bendera.

1

Akiwa na miaka 39, Macron anakuwa rais waumri mdogo zaidi wa kuchaguliwa kuwahi kuiongoza Ufaransa na wa kwanza kuchaguliwa kutoka nje ya vyama viwili vikubwa vya siasa nchini humo.

Katika taarifa yake, amesema kwamba Ufaransa imefanikiwa kufungua ukurasa mpya katika historia yake na kwamba alikuwa na ndoto ya kuwa mpiga mbiu wa nchi hiyo kwa kugunduliwa upya kwa matumaini na imani.

Mshndi huyo wa nafasi ya urais ametoa hotuba yale ya kwanza akiwa ni raisi mteule.

  • #SIBUKAMEDIA
  • #BBC SWAHILI.

 

 

Comments

comments