East Africa: nchi za EAC katika mikakati mpya ya kuongeza thamani ya mazao yao.

Rwanda, Uganda na Kenya zimejipanga kuongeza thamani ya mazao yao ya kilimo kama vile kupunguza hasara kwa bidhaa zinazoharibika haraka.

Mpango huu utawezeshwa na uwekezaji wa dola bilioni 2 kuweza kujenga vituo vya kuhifadhi bidhaa hizo.

kuanzishwa kwa mpango huu ni kutokana na hasara ambayo imeshuhudiwa baada ya mavuno kuharibika.

inakidiriwa kuwa zaidi ya asilimia 40 ya viazi, matunda, mboga uharibika kutokana na ukosefu wa hifadhi maalum ya kuhifadhi bidhaa kama hizi.

Dr Agnes Kalibata , rais wa AGRA , aliiambia gazeti moja la uganda kwamba mpango huu utawezesha wakulima kuwa na uwezo wa kupanda chochote wanataka na kuamua wakati wanataka kuleta mazao hayo kwa soko.

Na hatimaye wakulima wanatarajiwa kupata mapato zaidi.

Comments

comments