Donald Trump asema wafungwa hawafai kuachiliwa Guantanamo Bay.

_93218035_036730681-1

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amesema wafungwa zaidi hawafai kuachiliwa kutoka kwa gereza la Marekani la Guantanamo Bay, Cuba.

Amesema wafungwa waliosalia gerezani humo ni “watu hatari sana na hawafai kuruhusiwa kurejea kwenye uwanja wa mapigano tena”.

Rais Barack Obama alikuwa ameapa kuwa angefunga jela hiyo kabla ya kuondoka madarakani na amewahamisha wengi wa wafungwa waliokuwa wakizuiliwa humo.

Kwa sasa, wafungwa 60 wamesalia gerezani na ikulu ya White House ilisema baadaye Jumanne kwamba inapanga kuwahamisha wafungwa hao kabla ya tarehe 20 Januari.

Bw Trump alikuwa amepinga mpango wa Obama wa kufunga jela hiyo wakati wa kampeni.

Mwezi Februari alisema: “Asubuhi hii, nimemtazama Rais Obama akiongea kuhusu Gitmo, sawa, Guantanamo Bay, ambayo kusema kweli, ambayo kusema kweli, hatutaifunga.

#BBC SWAHILI

#SIBUKA MEDIA

Comments

comments